Kamati ya Bunge Utawala, Katiba na Sheria imependekeza serikali kutokuweka ulazima wa kufanya Wakurugenzi wa miji, majiji na halamashauri kuwa wasimamizi wa uchaguzi.

Akisoma taarifa hiyo, Mwenyekiti wa Kamati, Joseph Kizito Mhagama amependekeza kuwe na masharti mbadala.
“Kamati ilikuwa na maoni kwamba sheria isiweke ulazima kwa Mkurugenzi Mtendaji kusimamia uchaguzi badala yake kuwepo na masharti ya mtumishi wa umma mwandamizi au mtu mwingine yeyote mwenye sifa kuteuliwa kuwa msimamizi wa uchaguzi au msimamizi msaidizi wa uchaguzi,”