KAMATI YA FEDHA, UTAWALA TABORA YAKAGUA UTEKELEZAJI MIRADI YA MAENDELEO

Kamati ya Fedha na Utawala ya Halmashauri ya Manispaa ya Tabora imefanya ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo katika Kata za Ntalikwa, Ng’ambo na Ipuli, kwa lengo la kukagua maendeleo ya utekelezaji wa miradi hiyo. 

Katika Kata ya Ntalikwa, kamati imekagua ujenzi wa Shule Shikizi ya Kikundi huku Kata ya Ng’ambo, ukikaguliwa mradi wa vijana unaotekelezwa na Umoja Group, na Kata ya Ipuli, kamati ikitembelea Shule ya Msingi Ipuli na kukagua ujenzi wa madarasa mawili.

Aidha, kwa niaba ya Kamati ya Fedha na Utawala, Mwenyekiti wa Kamati hiyo ambaye pia ni Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Tabora, Gulamhussein D. Remtullah, amezipongeza Kamati za Ujenzi za madarasa hayo kwa usimamizi wa karibu na kuhakikisha mradi unakamilika kwa wakati.

Gulamhussein amesema usimamizi huo unapaswa kuwa mfano wa kuigwa na kamati nyingine, kwani pamoja na kukamilisha ujenzi kwa wakati, zimeweza pia kuongeza baadhi ya mahitaji muhimu katika mradi huo, hatua inayodhihirisha uwajibikaji na matumizi mazuri ya rasilimali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *