KAMATI TENDAJI YA YANGA SC YAJADILI UJENZI UWANJA WA KLABU

Wajumbe wa Kamati Tendaji wa Yanga SC, wamekutana visiwani Zanzibar kujadiliana ujenzi wa uwanja na suala la mwekezaji wa klabu hiyo.

Akizungumza katika mkutano huo uliofanyika Zanzibar hii leo Februari 14, 2026, Rais wa Yanga SC, Injinia Hersi Said amesema tayari wamewasilisha kwa GSM mahitaji uwanja wanaouhitaji.

Rais wa Klabu ya Soka ya Yanga, Injinia Hersi Said akizungumza jambo katika mkutano huo.

Amesema, “tunatambua yapo madaraja manne ya viwango vya viwanja vya CAF. Daraja la tatu ni uwanja ambao unaweza kuchezewa mpaka hatua ya robo fainali ya ligi ya mabingwa Afrika. Daraja la nne linaweza kuandaa mpaka hatua ya fainali. Tunalenga kuwa kati ya daraja la tatu na la nne la ubora wa viwanja.”

Hersa ameongeza kuwa, Yanga SC inamuhakikishia Rais wa GSM ushirikiano wa kutosha, wakitambua kiu ya mashabiki wao ambao wanatamani kuona wakimiliki uwanja wao.

Rais wa Makampuni ya GSM, Mfadhili na Mdhamini wa Klabu ya Yanga SC, Ghalib Said Mohamed akiwa katika mkutano wa majadiliano kati ya Kamati Maalum ya Ujenzi wa Uwanja na Mwekezaji unaofanyika Zanzibar.

“Niwahakikishie wananchi kuwa tunakwenda kuwa na uwanja bora na kisasa. Tunakwenda kuweka historia ya kuwa na kiwanja bora kabisa,” alisema Hersi.

Hersi amezidi kufafanua kuwa, “tunaenda kujenga uwanja ambao sio tu unahudumu mpira wa miguu pekee bali ni mradi ambao utakwenda kubeba majukumu mengine ya kijamii. Uwanja huu utakuwa na uwezo wa kutumika kwa ajili hafla na shughuli mbalimbali. Nawahakikisha tunakwenda kujenga uwanja ambayo unaakisi mandhari ya ubunifu utakao mudu mahitaji mbalimbali ya kijamii, sanaa, burudani na michezo.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *