KAMA UNA AINA HIZI ZA SIMU, WHATSAPP HAITOKUBALI TENA KWAKO……

Mtandao wa Kijamii maarufu zaidi duniani wa WhatsApp umetangaza rasmi kuondoa mtandao wao kwenye simu za zamani za Android ambazo hazipati maboresho ‘updates’ za mfumo mpya unaofanyika kila mwaka.

Simu ambazo hazitopata huduma ya WhatsApp ni pamoja na Samsung: zenye matoleo ya Galaxy S3, Galaxy Note 2, Galaxy Ace 3, Galaxy S4 Mini), kwa simu za Sony zenye matoleo ya Xperia Z, Xperia SP, Xperia T, Xperia V), kwa simu za LG ni zenye matoleo Optimus G, Nexus 4, G2 Mini, L90), kwa simu za Motorola ni zenye matoleo Moto G (1st Gen), Razr HD, Moto E 2014) na HTC ni zenye matoleo ya One X, One X+, Desire 500, Desire 601.

Taarifa ya WhatsApp imesema kuwa kuanzia Januari 01 2025, itaondoa huduma katika simu za aina hiyo lengo likiwa ni kuleta vipengele na huduma mpya zinazohitaji vifaa vya kisasa na kuachana kabisa na mifumo ya zamani.
Mbali na mtandao huo kuacha kufanya kazi katika Android lakini pia kwa watumiaji wa simu za Apple (Iphone) zenye mfumo wa iOS 15.1 mwisho wa kutumia mtandao huo ni mwezi Mei 2025.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *