KAHAMA WASHAURIWA KUPUNGUZA MATUMIZI DAWA ZA KUZUIA KUSHIKA MIMBA

Wanawake Wilayani Kahama mkoani Shinyanga, hasa wasichana wadogo wameshauriwa kupunguza matumizi ya dawa za kuzuia Kushika mimba almalufu P2 na badala yake watumie njia salama za uzazi wa mpango.

Wito huo umetolewa na Mratibu wa Huduma ya Afya ya Uzazi na Mtoto Manispaa ya Kahama,  Carolyne Boniventure wakati akizungumza na  Jambo Fm kuhusu matumizi ya dawa hizo kwa mabinti, hasa wanaosoma.

“Nitoe ushauri kwa wasichana na wanawake walio kwenye ndoa wapunguze matumizi ya dawa za kuzuia ushika mimba (P2)  na badala yake watumie njia sahihi za za uzazi wa mpango,” amesema Carolyne.

Aidha, amewataka wana ndoa kupanga uzazi kwa kuzaa watoto kwa mpangilio ikiwa ni Pamoja na kuwapishanisha kwa miaka miwili kabla ya kupata mtoto mwingine.

“Niwaombe kina baba na kina mama wapange uzazi wa mpango hawazuiliwi kuzaa watoto hata kumi ila wanatakiwa wazae kwa mpangilio na kwa kuwapishanisha walau miaka miwili ndipo upate mtoto mwingine” Ameongeza Carolyne.

Nao baadhi ya Wananchi wa Manispaa ya Kahama wameomba elimu izidi kutolewa kwa mabinti hasa  wa shule kuhusu madhara ya matumizi ya dawa hizo.

“Kiukweli elimu izidi kutolewa tu hasa kwa mabinti wetu walioko mashuleni kwani vijana wetu wamekuwa watumiaji wakubwa wa dawa hizi,sasa wapewe elimu ya madhara  ya dawa hizi, ” amesema Neema Moses na William Yanju. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *