Jamii imetakiwa kuwa na desturi ya kufanya uchunguzi pindi wanapohisi kuwa na changamoto ya kumeza chakula kwani hiyo inaweza kuwa dalili ya awali ya saratani ya koo la chakula.
Rai hiyo imetolewa na mkuu wa kitengo cha magonjwa ya mfumo wa chakula kutoka hospitali ya rufaa ya kanda Bugando Dk David Majige ambapo amesema kwa hapa nchini kuna wastani wa watu 9 kati ya watu laki moja wanaougua ugonjwa wa saratani ya koo la chakula na kwa kanda ya ziwa ni moja ya ugonjwa ambao unaokuja kwa kasi huku mkoa wa kagera ukiwa unaongoza kwa kanda hii kwa kuwa na wagonjwa wengi wa saratani hiyo.
Kwa upande wake daktari bingwa wa upasuaji na mfumo wa chakula kutoka katika hospitali ya rufaa ya kanda Bugando Dkt. Ahmed Binde amesema moja ya dalili za ugonjwa huo ni kushindwa kumeza chakula, kupaliwa pamoja na koo kuwasha na amewataka wananchi kuacha kutumia pombe zilizochanganywa (cocktail) ambazo hawajui mchanganyiko wake kwani nazo pia zinaweza kuleta majeraha kwenye koo.