Kadhi wa Mkoa wa Morogoro, Sheikh Mussa Bolingo amefariki dunia jana (Disemba 27) Ijumaa saa moja jioni wakati akipatiwa matibabu kwenye hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro.
Chanzo cha kifo cha Sheikh Bolingo kinasemekana ni ugonjwa wa kisukari wa muda mrefu, na alipelekwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro jana baada ya hali yake kubadilika zaidi.
Baada ya vikao vya familia na viongozi wa Baraza Kuu la Waislamu Tanznia (Bakwata) imeamuliwa kuwa Sheikh Bolingo atazikwa leo saa kumi jioni baada ya swala ya Alasiri katika eneo la msikitini wa Luqman uliopo maeneo ya Kihonda kwa Chambo Manispaa ya Morogoro.
Jambo FM inatoa pole kwa Baraza Kuu la Waislam Tanzania (Bakwata), Familia, Ndugu na Jamaa kwa kumpoteza Shekh Sheikh Mussa Bolingo.
inna lillahi wa inna ilayhi raji’un.