Kabla ya kusainiwa lebo ya Mavin, akiwa yupo anajitafuta Ayra Starr, aliwahi kuuza mboga mboga na matunda pamoja na bibi yake.
Mrembo huyo amebainisha hayo kupitia mtandao wa Instagram kwa kuandika “Nitashukuru Mungu milele kwa maisha niliyopitia. Mungu amenibariki sana, maana Miaka 6 iliyopita, nilikuwa nikiuza mboga na matunda na bibi yangu, tulikuwa tukiimba kwa yeyote anayetaka kunisikia, ila sasa watu wananilipa na kunitazama nikiwa natumbuiza.”