Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), limeutaarifu umma kuwa kumejitokeza baadhi ya watu wanaotumia mitandao ya kijamii kuweka maudhui yanayochochea kuliingiza Jeshi katika mambo ya siasa.
Kupitia taarifa iliyotolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano wa JWTZ, Kanali Bernard Masala Mlunga, imeeleza kuwa baadhi ya hoja hizo zinatolewa na watu waliopo katika mazingira ya kijeshi, kujinasibisha na Jeshi, walioachishwa Jeshi kwa tabia na mwenendo mbaya pamoja na kujihusisha na siasa na uanaharakati.




