JWTZ LAWAONYA WANAHARAKATI WACHOCHEZI, LAGUSIA HALI YA ULINZI NA USALAMA

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limetoa tamko rasmi likieleza kuwa linaendelea kufuatilia kwa karibu hali ya Ulinzi na Usalama nchini katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 28-29, 2025, kama ilivyotangazwa na Tume Huru ya Uchaguzi ya Taifa (INEC) na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa hii leo Oktoba 15 2025 na Kaimu Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano wa JWTZ, Kanali Bernard Masala Mlunga, Jeshi limeeleza kuwa kwa ujumla linaridhishwa na hali ya usalama nchini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *