Msanii wa Canada, Justin Bieber na mke wake Hailey Bieber wanaadhimisha miaka mitano ya ndoa yao takatifu.
Bieber ameandika kwenye ukurasa wake wa instagram “Mpenzi wangu,” “Miaka 5. Umeuteka moyo wangu. Najua kutoka kwenye kina cha nafsi yangu hadi mifupani mwangu kwamba safari hii pamoja nawe itazidi matarajio yetu makubwa zaidi.”
Justin na Hailey Bieber walichumbiana mnamo 2014, na kuachana, cha kushangaza miaka miwili baadaye, Justin na Hailey Bieber walianza tena penzi lao na wakachumbiana tena mwaka wa 2018 na hatimaye Justin na Hailey Bieber walifunga ndoa katika mahakama mnamo Septemba 13, 2018.
Harusi hiyo ilihudhuriwa na watu wengi wakiwemo nyota kama Kris Jenner, Kylie na Kendall Jenner, mwanamitindo Joan Smalls, Justine Skye pamoja na rafiki yake Jaden Smith.