Jambo La Leo

Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Jumla ya Bilioni 216 zatumika kulipa nauli za watumishi

Naibu Waziri Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora),
Ridhiwani Kikwete amesema kiasi cha Sh bilioni 216 kimetumika kulipa malimbikizo ya madai ya watumishi waliokwenda likizo bila kupewa nauli kwa wakati.

Ametoa kauli hiyo alipokuwa akijibu swali la nyongeza la mbunge wa Viti Maalumu, Mariam Kisangi aliyetaka kuju serikali inatatuaje changamoto ya baadhi ya walimu wanaoenda likizo bila ya kupewa nauli.

Akijibu swali hilo Naibu Waziri huyo amesema Serikali imewalipa watumishi 126,924 na kuongeza kuwa serikali imekuwa ikipokea malalamiko hayo kuhusu malimbikizo ya madai, lakini tayari imeshalipa kiasi hicho cha fedha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *