Msanii mkongwe wa muziki kutoka nchini Kenya, Jua Cali, amedai kuwa wasanii wa Tanzania wanafanya shoo sana Kenya kwa sababu Kenya kuna pesa nyingi kuliko Tanzania.
Jua cali amesema hayo kupitia mahojiano aliyofanya na waandishi wa habari hivi karibuni.
Mkongwe huyo pia akaongeza kuwa Kenya wasanii zaidi ya 15 wanafanya Shoo ndani na nje ya nchi, lakini Tanzania ni wasanii wawili tu.