Jose Chameleone ametangaza tamasha la yeye na ndugu zake ambao ni Pallaso na Weasel, ifikapo Desemba 15 mwaka huu. Na tamasha hilo limepewa jina la’ Mayanja Brothers Live in Kololo Airstrip’.

Chameleone ambaye jina lake halisi ni Joseph Mayanja ametangaza taarifa hiyo wakati wa kumbukizi ya kuzaliwa mdogo wake aitwaye Pallaso Mayanja, Septemba 5.