JOEL MBOYI ACHUKUA FOMU KUWANIA UBUNGE JIMBO LA KISESA

Na Saada Almasi – Meatu.

Mwekezaji na mmiliki wa kampuni ya City Property yenye matawi yake Dar es Salaam, Dodoma na Morogoro, Joel Mchungwa Mboyi amechukua fomu ya kuwania ubunge katika jimbo la Kisesa wilayani Meatu mkoani Simiyu

Hii imekuwa ni mara ya kwanza kwa Joel kuwania nafasi hii huku akiwa kijana wa umri wa miaka 31 na akisadikiwa kuwa ndiye mgombea mwenye umri mdogo kuwania nafasi hiyo katika jimbo hilo.

Akiwa mzaliwa kijiji cha Mwakasumbi kata ya Mwabuma ndani ya jimbo la Kisesa Joel ambaye ni kada wa chama cha mapinduzi CCM amechukua fomu na kukabidhiwa na katibu wa wilaya ya Meatu Naboth Manyonyi katika ofisi za chama hicho wilayani Meatu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *