JMAT yatoa tamka kuhusu Bandari

Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT) imepaza sauti na kuwataka watanzania katika kada tofauti zikiwemo zile za dini na siasa kuiachia serikali swala la bandari kwani wao ndio wenye maamuzi ya mwisho.

Rai hiyo imetolewa leo Agosti 25 jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti Taifa wa Jumuiya ya maridhiano na Amani Tanzania (JMAT) Sheikh Alhad Salum.

Shekhe Salum amesema kuwa hakuna haja ya kuleta majibizano na kuleta tofauti kuhusiana na mitazamo tofauti ya kuhusiana na kadhia ya bandari kwani kufanya hivyo kunaweza kukazalisha migogoro isiyo na faida nchini.

Amesema watanzania wanatakiwa waiamini serikali yao kwa maslahi mapana ya nchi ikimiendelee na jambo hilo kwa namna bora.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *