Jambo La Leo

Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

JKT watakiwa kujua thamani yao

Wahitimu wa mafunzo katika ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) wametakiwa kutambua thamani zao na jinsi Serikali inavyowajali katika kuboresha hali zao za kiuchumi na taifa kwani Serikali haitamani kuona jitihada na nguvu ilizoweka kwao zinaishia njiani.

Hayo yamesemwa leo Disemba 8, 2023jijini Dodoma na Waziri wa Kilimo Hussein Bashe wakati akifunga mafunzo ya JKT kundi maalum la Jenga kesho iliyo bora (BBT) kikosi cha 834 Makutopola ikiwa ni oparesheni maalum ya miaka 60 ya Jeshi hilo.

Aidha Waziri Bashe amewahasa wananchi kuona fursa zilizopo kwenye kilimo kwani kimekuwa uti wa mgongo pamoja na kutoa rai kwa vijana kuchangamkia fursa pale wanapozipata na kuzitumia kutimiza malengo yao.

Kwa upande wake Mkuu wa JKT Meja Jenerali Rajabu Mabele ametoa rai kwa taasisi zingine kuona umuhimu wa mafunzo hayo kwa watendaji wao kwani yanalenga kuwajengea vijana uzalendo kwa taifa lao, nidhamu nzuri, hali ya kufanya kazi bila kuchoka, umoja na mshikamano pamoja na uvumilivu wanapopambana na changamoto za kikazi na maisha.

Naye Kaimu kamanda kikosi 834 kikosi cha jeshi Meja James Macheta amesema kuwa mafunzo hayo waliyo yapata vijana yatawasidia katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku na kwa taifa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *