Uongozi wa JKT Tanzania rasmi umethibisha kikosi chao kitautumia Uwanja wa CCM Kambarage Mjini Shinyanga kama uwanja wao wa nyumbani katika michezo yote ya Ligu Kuu Tanzania Bara hadi pale uwanja wao wa Meja Jenerali Isamuyo uliopo Mbweni Dar es salaam utakapokamilika baada ya matengenezo makubwa yanayoendelea kufanywa.
Hayo yameelezwa na Afisa Habari na Mawasiliano wa JKT Tanzania, Masau Bwire katika Mkutano wake na vyombo vya habari uliofanyika leo Jumatano (Septemba 27) Mjini Shinyanga.
Masau amesema wameamua kuuchagua uwanja wa CCM Kambarage kama uwanja wao wa nyumbani kwani wanataka maeneo yote nchini yapate fursa ya kushuhudia Soka, hivyo furaha ya JKT Tanzania ni kuona wakazi wa Shinyanga wanapata furaha ya Soka hivyo amewaomba wakazi wa Mkoa huo kuipa ushirikiano timu yao