Jezi ya staa wa Soka Argentina, Lionel Messi inatarajiwa kuwa kwenye mnada wa seti ya jezi sita alizotumia kwenye Kombe la Dunia mwaka 2022 huko Qatar, ambao kwa mujibu wa Sotheby, mnada huo utafunguliwa Novemba 30, 2023 hadi Desemba 14 Jijini New York-Marekani.
Katika mnada huo jezi zinatarajiwa kuuzwa kwa zaidi ya USD milioni 10 (Tsh. bilioni 24.9).
Jezi hizo ni zile zilizovaliwa na La Pulga wakati wa kila hatua ya michuano ya Kombe la Dunia ambapo kama mnada utakwenda kama ulivyopangwa, bei ya seti ya jezi za Messi itapita jezi iliyovaliwa na staa wa mpira wa kikapu Michael Jordan.
Jezi iliyovaliwa na Messi yenye thamani kubwa zaidi kwenye maisha yake ya soka iliuzwa kwa dola $450,000 (Tsh. bilioni 1.1) ilikuwa ni jezi aliyoivaa wakati wa mchuano wa El Clásico mwaka 2017 alipokuwa akichezea FC Barcelona dhidi ya Real Madrid ya Cristiano Ronaldo.