
Polisi Mkoa wa Iringa linawasaka Askari namba F.4987 Sajenti Rogers wa Kituo cha Polisi Ipogolo na Askari wa Jeshi la Akiba (Mgambo) aitwaye Thomas Mkembela kwa tuhuma za kumuua Nashon Kiyeyeu (23) Mkazi wa Nyamhanga Manispaa ya Iringa.
Chanzo cha mauaji hayo, inadaiwa Disemba 14, 2024 Sajenti Rogers alipokea taarifa kutoka kwa mwananchi mmoja ambaye hakumtaja kwa jina kuwa anamtuhumu Nashon Kiyeyeu kuwa amemwibia simu yake. Sajenti Rogers kwa kushirikiana na huyo Mgambo walimkamata mtuhumia na inadaiwa walimpiga na walipoona amepoteza fahamu walimpeleka Hospitali moja binafsi na baadaye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa na ikabainika ameshafariki dunia.
Baada ya kuona hivyo walitoweka na kukimbilia kusikojulikana. Polisi Mkoa wa Iringa inaendelea na mako mkali wa kuwatafuta watuhumiwa hao pamoja na kusambaza taarifa Mikoa mbalimbali.


