
Jeshi la polisi mkoa wa Mwanza limefanikiwa kudhibiti maandamano ya wanachama wa chama cha Demokrasia na Maendeleo- CHADEMA yaliyokuwa yamepangwa kufanyika leo February 19.2025 katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Mwanza hasa katika wilaya ya Ilemela na Nyamagana.
Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza DCP. Wilbrod Mutafungwa amesema maandamano hayo yaliyopangwa kufanyika hayakuwa na uhalali wa kisheria hivyo Jeshi la polisi mkoa wa Mwanza lilijipanga kuyadhibiti kwa kufanya doria maeneo mbalimbali ya jiji la Mwanza kuhakikisha hakuna vurugu ama maandamano yoyote yanayoweza kuleta uvunjivu wa Amani kwa wananchi ; na Jeshi la polisi halitasita kumchukulia mtu au kikundi cha watu hatua za kisheria watakao andamana kinyume na sheria.
Naye Mkuu wa mkoa wa Mwanza Said Mtanda amewataka wanachama wa chama cha Demokrasia na Maendeleo- CHADEMA pamoja na wananchi kutii sheria na kutoa ushirikiano kwa Jeshi la polisi na vyombo vingine vya usalama ili kufanikisha uchunguzi na upatikanaji wa mwanachama huyo anaedaiwa kupotea tarehe 14.2.2025 ; na kwamba serikali ipo macho kuhakikisha usalama wa raia na mali zao unakuwa salama.
Sambamba na hayo, Katibu wa CHADEMA mkoa wa Mwanza Boniphace Nkobe amewataka wanachama wa CHADEMA kuwa watulivu na kutoa ushirikiano kwa Jeshi la polisi na Serikali ili kuhakikisha mwanachama wao anapatikana akiwa salama.