Jeshi la Polisi limefanikiwa kumkamata mtuhumiwa aliyewatapeli watalii

Jeshi la Polisi limesema limefanikiwa kumkamata mtuhumiwa aliyewatapeli watalii walikuja nchini kwa ajili ya kupanda mlima Kilimanjaro huku likibainisha kuwa Tanzania ni nchi salama kwa wageni wa ndani na nje ya Tanzania.

Hayo yamsemwa na Kamnda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro kamishna msaidizi wa Polisi ACP Simon Maigwa leo katika lango la mweka ambalo hutumika kushuka kutoka katika mlima Kilimanjaro ambao ni mlima mrefu barani afrika.

Ameongeza kuwa mtuhumiwa aliyekamatwa jina jina lake limehifadhiwa kwa sababu za kiupelezi huku akibanisha kuwa mtuhumiwa anatoka nje ya Tanzania,huku akiwaomba watalii hao kuendelea kuwa mabalozi wazuri wa kuitangaza Tanzania.

Amewapongeza watalii hao zaidi ya thelathini kwa namna walivyo kitangaza kituo cha Polisi Utalii na Diplomasia Arusha na Kilimanjaro kwa kupandisha bango linaloaiambia dunia kuwa Tanzania ni mahala salama kwa utalii na kutembelea.

Kwa upande wake bwana Chris Lomas ambae ni Mkurungenzi wa kampuni ya hope for love amewashuru serikali na Jeshi la Polisi kwa namna ambavyo wamelifuatilia swala lao hatu moja baada ya nyingne na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa aliye watapeli.

Nae bwana Oscar Mosha ambaye Mkurungenzi msaidizi wa kampuni ya utalii ya Tanzania Escapade ambayo inashughulika na kuwapandisha watalii katika mlima Kilimanjaro amewashukuru watalii hao kwa kuchagua kuja Tanzania na kuapanda mlima Kilimanjaro huku akiwa waambia Tnaznia ni sehemu salama kwa utalii.

Franke Alexnder ambaye ni Afisa mtalii Mkuu kanda ya kaskazini amewapole kwa kilichotokea huku akiwa wakiwakikishia Tanzania ni salama.

Mkuu wa kituo cha Polisi utalii na Dipolomasia Mrakibu wa Polisi SP Waziri Tenga amesema Tanzania ni salama na Kilimanjaro ni salama ambapo amewaambia wasjikie wako salama.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *