Jeshi la Polisi latoa onyo kwa wanaojiteka.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi limesema litaendelea kuchukua hatua kali za kisheria dhidi ya wananchi wenye tabia ya kujiteka kisha kupiga simu kwa ndugu zao kuhitaji pesa wakidai watekaji ndio wanaohitaji pesa hizo jambo ambalo linaleta taharuki katika jamii na serikali.


Kauli hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Richard Thadei Mchomvu wakati akitoa ufafanuzi wa video clip iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii ikidai Jeshi hilo limeshindwa kumpata kijana aliyetekwa.


Kamanda Mchomvu amesema tukio la kutoweka kwa kijana huyo liliripotiwa tarehe 07 Februari 2024 katika kituo cha Polisi Mazizini, ambapo baada ya kupokea taarifa hiyo ufuatiliaji wa simu iliyofanya mawasiliano ulianza na kufanikiwa kubaini alipo kijana huyo.


Kijana huyo alitumiwa fedha shilingi laki mbili na kaka yake wakiamini kwamba wanawatumia watekaji na baada ya siku tatu kijana huyo alipatikana, alipohojiwa alieleza kwamba hakutekwa bali alijiteka ili apate fedha za kuanzia mtaji wa huduna za kifedha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *