JESHI LA POLISI DODOMA LAKAMATA GARI, PIKIPIKI 31, BANGI KILO 10, TV, RADIO NA ‘PANYA ROAD’….

Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma limesema katika operesheni zake za hivi karibuni walizofanya wamekamata jumla yapikipiki 31 zinazozaniwa kuwa za wizi, bangi kilo 10, mirungi kilo 10, Tv, Radio na gari.

Hayo yamebainishwa leo Desemba 23,2024 Jijini Dodoma na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma George Katabazi wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hali ya usalama mkoa wa Dodoma kuelekea sikukuu.

RPC Katabazi amewataka pia wananchi kujitokeza kwa wingi kutambua mali hizo wakiwa na nyaraka halali, mbali na hiyo Katabazi amesema ‘Tumefanikiwa kukamata kijana mmoja kati ya watatu waliokuwa wakisakwa na jeshi la polisi wakidhaniwa kuwa ni “panya road”. Tunaendelea kusisitiza wananchi kutii sheria bila shuruti na kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi’. – Katabazi

Katika hatua nyingiine Jeshi la Polisi limewahiza wananchi kujiepusha na matumizi ya pombe kupitiliza wakati wa sikukuu kwa faida za usalama wao na watu wengine.

Amesema kipindi cha sikukuu mara nyingi huambatana na matukio ya ajali, ugomvi na matukio mengine yasiyofaa kutokana na ulevi uliopitiliza.

“Kuna tabia ambayo inazuka wakati wa sherehe watu wanajisahau wanakunywa pombe kupitiliza matokeo yake wanasababisha kuingia katika hatari ya kusabisha ajali ambazo nizakujitakia na kuvamiwa’. – Katabazi.

Ameongeza kuwa :”Tunatoa rai kwa wananchi wote kusherekea sikukuu kwa amani na utulivu.Kila mmoja ahakikishe anakunywa kwa kiasi na kwa wanaosafiri na madereva kuhakikisha wanaepuka matumizi ya vileo’. – Katabazi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *