Jela miaka 30 kwa kumbaka mtoto wake

Mkazi wa Kijiji cha Nyamizeze wilayani Sengerema mkoani Mwanza, Samson Mibulo (35) amehukumiwa kwenda jela miaka 30 baada kukiri kosa la kubaka.

Hukumu hiyo ya kesi ya jinai namba 122/2023, imetolewa leo tarehe 02 Novemba, 2023 na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya wilaya ya Sengerema, Evod Kisoka.

Awali, akisoma maelezo ya kosa hilo mbele ya hakimu, wakili wa Serikali, Morice Mtoi amsema mshitakiwa alitenda kosa hilo kwa mhanga akiwa ni baba yake mlezi kwa nyakati tofauti mwezi Oktoba 2023 nyumbani kwake kijiji cha Nyamizeze na kukamatwa tarehe 23/10/2023 na Mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai wa Wilaya ya Sengerema, Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP) Tito Mohe baada ya kupata taarifa toka kwa wasamaria wema.

Pamoja na maombi ya mshtakiwa (Mibulo) kuomba kupunguziwa adhabu, Mahakama imemhukumu kifungo hicho cha miaka 30 ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *