Jela Miaka 20 kwa kukutwa na Hatia ya Mauaji ya Kimbari Rwanda

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa vyombo vya habari vyenye uhusiano na serikali,Mahakama nchini Rwanda imemkuta na hatia Venant Rutunga ya kushiriki mauaji ya kimbari ya mwaka 1994, na kumuhukumu kifungo cha miaka 20 jela.

Venant Rutunga mwenye miaka 75, alirudishwa Rwanda kutoka Uholanzi mwaka 2021 alikofunguliwa mashitaka kuhusiana na madai kwamba aliagiza kufanyika mauaji hayo zaidi ya robo karne iliyopita.

Kulingana na mwendesha mashitaka, Rutunga ambaye amewahi kuwa Mkurugenzi wa Kikanda wa taasisi ya ISAR aliwapeleka polisi kwenye taasisi ya utafiti wa kilimo kulikokuwa na wafanyakazi wa Kitutsi na watu wengine waliokuwa wamejificha, ambao wote waliuawa.

Rutunga, aliyekana mashtaka  alidai kuwa aliwaita maafisa hao ili kulinda usalama, uamuzi ambao alisema uliidhinishwa na bodi ya wakurugenzi ya ISAR.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *