Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Jela maisha kwa kumbaka mtoto kwa zamu

Mahakama ya Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga imewahukumu Watu wawili Kulwa Lugiko( 28) na Jeremiah Machunda (18), wakazi wa kijiji cha Nyamishiga Halmashauri ya Msalala kifungo na kutumikia adhabu ya kwenda Jela Maisha kwa kosa la kumbaka na kulawiti Mtoto wa Miaka 12.

Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Kahama, Christina Chovenye ambapo amesema washtakiwa hao wamekutwa na hatia kwa makosa hayo mawili kila mmoja kinyume na kifungu cha Sheria namba 131 (1)(2)(e) na 131(1), na 154(1)(a) kilichofanyiwa marekebisho Mwaka 2022.

Washtakiwa wametenda Makosa hayo Julai 2023 katika kijiji cha Nyamishga ambapo kwa mujibu wa sheria, Jeremia amehukumiwa kuchapwa Viboko 6,kulipa fidia ya Laki 5 na kwenda jela Maisha wakati Kulwa Lugiko amehukumiwa kutumikia Miaka 30 na kifungo cha Maisha Jela.

Kwa mujibu wa Mwendesha Mashtaka Inspekta Evodia Bahimu ameiambia Mahakama kuwa watuhumiwa wamekuwa wakimfanyia kitendo hicho mhanga kwa zamu kwa kubadilishana majira, Jeremiah akidaiwa akifanya Mchana na Kulwa Usiku kwa vipindi na muda tofautitofauti katika Mwezi huo wa 7.

Walipotakiwa kujitetea Washtakiwa hawakuwa na maelezo yoyote ya kujibu hivyo kuifanya Mahakama itoe hukumu dhidi yao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *