Kupitia Instastory yake staa wa muziki Jay Melody ametangaza kuacha muziki, ameandika “ Ninaacha muziki”, kisha kuweka alama ya kushukuru.
Chanzo cha maamuzi ya msanii huyo, kuacha muziki bado hakijafahamika na hivi karibuni amefanya kolabo na msanii wa muziki Phina na miezi mitatu iliyopita alichia ngoma iitwayo ‘Mbali na Wewe” ambayo inawatazamaji Milioni 5.3 YouTube.