
Staa wa Muziki wa Bongo Fleva Jaymelody leo kupitia ukurasa wake wa instagram amemtolea uvivu Mwanamitandao na Mtangazaji Mwinjaku kwa kile alichosema kumsema vibaya.
Kwenye post yake Jay melody ameandika ‘Kwenye hii tasnia ubaya ni kwamba unapambana sana mpaka unafika sehemu watu wanakuelewa lakini watu wanatumia dakika chache tu kutaka kuharibu juhudi zako zote ulizozifanya, kibaya zaidi tunadharaulika wakati tunapambana kuja kwenye mafanikio hakuna mtu anayejali’ – Jay Melody
‘Nimejitahidi kumuheshimu kila mtu kwa nafasi yake ingawa najua siwezi kumridhisha kila mmoja lakini najitahidi sana kujiweka mbali na matatizo. Nilichogundua hata uwe mwema kiasi gani kwa baadhi ya watu ndio kwanza unadharaulika na hao hao watatumia kukuona kama we bado sana kisa tu umewapa nafasi ya kuwa sehemu ya maisha yako.’ – Jay Melody
‘Mimi naheshimu sana kazi zangu na za wasanii wenzangu kitendo cha kusema kufanya kazi na @diamondplatnumzkimenishusha najua hakuna aliyekua anaona kama inawezekana lakini juhudi zangu ndo zimefanya kaka yangu kuona nastahili kukaa kwenye kazi yake na naliheshimu hilo.’- Jay Melody.

‘Ni kawaida yangu kupambana vita zote nazopigwa kimyakimya lakini ukimya wangu usiwe sababu ya watu kuongea wanavotaka jamani.Mziki ni kazi kama kazi nyingine una stress unahitaji umakini pia. Sasa hawa watu wanaokuja kutuongelea vibaya huku nia yao nini, tudate muaze kutusema vibaya,sijapendezwa hata kidogo na ujue kwamba ukimdhalilisha mtu hili ni deni utalilipa.’ – Jay Melody.
‘Sijawahi kusema wala kuongea ila sasa imekua too much ni kama kuna watu wanaona hii nafasi sistahili wakati mwingine unakutana na mtu kwa mara ya kwanza lakini tayari yeye kashajipanga jinsi ya kukupokea mtu anakuvimbia ukiamua na wewe ukae kimya utasikia anajisikia daaah mpaka najiulizaga kwani hua mnaambiwaga nini jamani.Mimi ukiacha kua msanii mkumbuke na mimi pia ni binadamu na siko kamili kama watu wengine msinifanye ivo jamani’ – Jay Melody.
‘Mwisho kabisa kulikua hakuna haja ya kuniongelea mimi vibaya.
Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa hizi hatua zangu,
Lakini pia nashukuru mashabiki zangu kwa kuendelea kunisupport.🙏’ – Jay Melody.


