JANGA LA MOTO SINGIDA: SHEIKH WA MKOA AWAPA POLE WAFANYABIASHARA, RC DENDEGO

Na Saulo Stephen – Singida.

Kufuatia kutokea kwa Janga la Moto uliozuka usiku wa kuamkia leo na kuteketeza maduka ya wafanyabiashara katika soko kuu la mkoa wa Singida, Shekh wa Mkoa wa Singida Issa Nassor ametoa pole kwa Mkuu wa Mkoa huo Halima Dendego pamoja na wafanyabiashara walipata kutokana hasara kuteketea kwa mali zao katika soko.

Shekh Issa Nassor ametoa pole hizo wakati akizungumza na Jambo fm ofisini, ambapo amesema kuungua kwa maduka hayo katika soko hilo nipigo kubwa kwa Wafanyabiashara pamoja na wananchi wa mkoa wa Singida kwani soko hilo ni sehemu muhimu katika uchumi wa mkoa wa Singida.

Aidha amewataka wafanyabiashara walipata hasara kutoka na mali zao kuteketezwa na moto kuwa na subra kwani katika kipindi ambacho subra inahitajika zaidi ni kipindi cha shida na nyakati na Wala si kipindi cha furaha, hivyo wanakila sababu ya kuwa watulivu na kumshukuru mwenyezi Mungu kwa Jambo hilo ambalo limetokea katika Biashara zao.

Sanjari na hayo Shekh huyo wa mkoa wa Singida amewapongeza wananchi wa mkoa wa Singida kwa kutoongiwa na tamaa wakati wa zoezi la ukoajia hali iliyopelekea mali zilizookolewa kuwa salama na kutokuwepo wizi wa aina yeyote.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *