JAMUKAYA RAMADHANI CUP 2025 YAZINDULIWA RASMI SHINYANGA..

NA EUNICE KANUMBA -SHINYANGA 

MASHINDANO ya Jamukaya Ramadhan Cup 2025, yamezinduliwa rasmi na Kampuni ya Jambo Group na yanatarajiwa kufanyika mwanzoni mwa mwezi Machi mwaka huu, katika kipindi cha Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Michuano hiyo inayojivunia kuunganishwa na tamaduni za kidini ya kiislamu  itaendelea kuhamasisha umoja na mshikamano katika jamii, ikiwa na kauli mbiu ya mwaka huu: “Jamukaya Ramadhani cup hii ni ibada tuungane na tushiriki kwa pamoja “

Uzinduzi huo umefanywa na Msimamizi wa Chapa wa kampuni ya  Jambo Group ambae pia ni  Meneja Mkuu wa Jambo Media, Nickson George, na kuzungumza na waandishi wa  habari moja kwa moja   leo, Januari 31, 2025 kupitia kipindi cha michezo cha WARM UP kinachoruka hewani kupitia jambo fm kila kuanzia saa nne asubuhi hadi saa sita mchana kuanzia jumatatu hadi ijumaa.

Mashindano yameboreshwa zaidi kwa Mwaka 2025!

Akizungumza wakati wa uzinduzi, George amesema kuwa mashindano ya mwaka huu yatafanyika usiku kuanzia saa 4 katika uwanja wa Chuo cha Ualimu Shinyanga (Shycom), na yatatoa fursa ya kipekee kwa jamii kuungana na kufurahi pamoja wakati wa mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

“Kutakuwa na timu 20 za mpira wa miguu zinazoshiriki, ikijumuisha timu 16 zilizoshiriki michuano hiyo  mwaka 2024, huku zawadi kwa mshindi wa kwanza kwa mwaka huu 2025  zikiwa zimeongezeka kutoka shilingi milioni 1 hadi shilingi milioni 5,” amesema George.

Kwa mujibu wa George, timu zinakaribishwa kujiandikisha kuanzia leo, tarehe 31 january 2025  huku kiingilio cha timu kikiwa sh. 300,000/= kwa timu za kawaida na sh. 500,000/= kwa timu za mashirika.

Kwa wananchi, viingilio vimepangwa kuwa sh. 1,000/=, na kila mtazamaji atapata kinywaji cha Jambo mlangoni.

Fursa za Kiuchumi na Umoja wa Jamii

Amesema mashindano haya hayataishia tu uwanjani, bali pia yataleta fursa kubwa kwa wajasiriamali wa Shinyanga. 

“Wajasiriamali wataweza kufanya biashara zao kwa kiingilio kidogo cha sh. 1,000, ambapo wataweza kuuza bidhaa mbalimbali kwa umma unaohudhuria mashindano,” ameongeza George.

Amefafanua kuwa, Jamukaya Ramadhan Cup pia inalenga kukuza afya na ustawi wa kijamii katika kipindi cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, ambapo michezo itakuwa njia ya kuimarisha umoja na mshikamano katika jamii.

“Katika kipindi hiki cha mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, wachezaji na mashabiki wataweza kupata nafasi ya kuburudika na kuungana kupitia michezo, huku wakijikita katika ibada na kumtumikia Mwenyezi Mungu,” amesema George.

Taa Angavu, Ulinzi na Usalama Upo!

Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano hayo, Jerry Julius, amesisitiza kuwa kamati imejipanga vyema kuhakikisha mashindano haya yanaendeshwa kwa ufanisi.

 “Mapungufu ya mwaka 2024 tumeyafanyia kazi na tumeboresha miundombinu, ikiwa ni pamoja na kuweka taa angavu zaidi uwanjani.

 U”Katika kipindi hiki cha mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, wachezaji na mashabiki wataweza kupata nafasi ya kuburudika na kuungana kupitia michezo, huku wakijikita katika ibada na kumtumikia Mwenyezi Mungu,” amesema George.

Taa Angavu, Ulinzi na Usalama Upo!

Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano hayo, Jerry Julius, amesisitiza kuwa kamati imejipanga vyema kuhakikisha mashindano haya yanaendeshwa kwa ufanisi.

 “Mapungufu ya mwaka 2024 tumeyafanyia kazi na tumeboresha miundombinu, ikiwa ni pamoja na kuweka taa angavu zaidi uwanjani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *