JAMBO FM YAPOKEA CHETI CHA PONGEZI KUTOKA MAHAKAMA KUU

Na Eunice Kanumba- Shinyanga.

Mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Shinyanga, imekabidhi cheti cha pongezi kwa Jambo Fm  kutokaba na mchango wake wa kuripoti kwa weledi Habari za Mahakamani kwa mwaka 2024 pamoja na ushiriki wake wa kina katika maadhimisho ya wiki ya sheria mwaka 2025

Hafla ya utoaji wa Vyeti hivyo, imefanyika katika ukumbi wa Mahakama Kuu Mkoani Shinyanga lengo likiwa ni kuthamini juhudi za wadau mbalimbali waliowezesha kufanikiwa kwa maadhimisho ya wiki ya sheria.

Katika hafla hiyo, Jambo Fm ilielezewa kuwa ninkituo bora ambacho kimekuwa na mchango wa kipekee katika kuhabarisha jamii kuhusu shughuli za Mahakama na kuimarisha mahusuiano kati ya muhimili huo na Wananchi.

Wakipokea cheti hicho, Jambo Fm imehaidi kuendelea kushirikiana na wadau mbalimbali na jamii kwa ujumla, katika kuhakikisha Wananchi wanafikiwa na taarifa sahihi, kwa wakati na kwa ufanisi.

Ni mara ya pili mfululizo sasa kwa Jambo Fm kupokea cheti hicho ambapo kwa mara ya kwanza ilikuwa ni katika maadhimisho ya mwaka 2024 na kuonesha namna kituo hicho kinavyoendelea kuwa sehemu muhimu ya kuelimisha na kuhabarisha Umma kuhusu masuala ya Sheria na Haki

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *