Meneja Mkuu wa Jambo Media, Bwana. Nikson George amefungua milango rasmi kwa msikilizaji na mdau wa burudani kanda ya ziwa mwenye uwezo na hadhi ya ukubwa wa chapa yaJambo fm 92.7 kutumia na kuchangamkia fursa ya udalali ya kuiuza jambo fm na kumtafuta dalali mwenye fani hiyo ya kuifanya jambo kuendelea kuwa na maisha fresh.

Nickson George amesema dalali atakayekuwa tayari kuiuza Jambo fm ni lazima awe • mkazi wa mkoa wa shinyanga na wilaya zake.
• Awe na elimu, ufahamu na uelewa wa masoko
• Awe na lugha yenye ushawishi
• Mwenye umri kuanzia miaka 18 na kuendelea
• Awe na uwezo wa kuzungumza kiswahili na kingereza
• Awe wa kike au wa kiume.
Akiongelea namna ya kuomba kazi hiyo ya udalali amesema muombaji anaweza kutuma cv au wasifu wake kupitia barua pepe ambayo ni info@jambofm.co.tz au anaweza kuiwasilisha moja kwa moja kwenye ofisi zetu zilizopo Ibadakuli. mwisho wa kupokea maombi ni Agosti 25, 2023 saa 12 jioni.