JAMBO AKABIDHI VIFAA VYA MICHEZO MEATU JOGGING CLUB

Na Saada Almasi, Meatu – Simiyu.

Katika kuendelea kuboresha mazingira ya michezo na kuhamasisha watu wengi kujiunga na michezo wilayani Meatu mkoani Simiyu ,mbunge wa jimbo hilo Salum Khamis Salum ametoa vifaa vya michezo kwa wanachama wa Meatu Jogging Club ambavyo watavitumia katika kipindi chote cha mazoezi.

Akikabidhi vifaa hivyo nyumbani kwake Salum amesema kuwa anafurahishwa na kujitoa kwao kufanya mazoezi na kwamba hatua hiyo ni katika kutimiza ahadi yake ya kipindi cha uchaguzi ya kuboresha mazingira ya michezo wilayani humo.

“niliahidi kuwasaidia kwa hali na mali na huu ni mwanzo mengi mazuri yanakuja,ninachohitaji kutoka kwenu ni kuhamasisha zaidi watu kujiunga na klabu yenu kwani mazoezi ni afya na msisite kuniambia kila mwanachama mpya ambaye atajiunga nitampatia vifaa,” alisema.

Ameongeza kuwa, hatoishia kuunga mkono klabu hiyo bali hata timu nyingine ambazo zinahitaji msaada wake atahakikisha zimesonga mbele na kuifanya wilaya hiyo kuwa ya mfano kimichezo.

Akipokea vifaa hivyo, Afisa Michezo wa Halmashauri hiyo, Hassan Senguro amemshukuru Jambo kwa kutimiza ahadi yake huku akimuahidi kuhamasisha watu wengi zaidi kujiunga na klabu hiyo.

Ameasma, “kipekee nitoe shukrani zangu za dhati kwani ulituahidi na umetimiza ahadi yako ninaimani vifaa hivi  tutavitumia kufikisha ujumbe wa afya kwa kila mshiriki na kuwavutia wengi Zaidi kujiunga kama ilivyo kawada kila jumamosi tunajumuika pamoja hatutochoka na nina hakika tutaongeza wanachama zaidi.”

2 responses to “JAMBO AKABIDHI VIFAA VYA MICHEZO MEATU JOGGING CLUB”

  1. Hongera sana Mhe.Salum Khamis Salum(Jambo) wewe ni Kiongozi wa Vitendo zaidi kuliko maneneo na Mwenyezi Mungu akuongoze katika kipindi chako cha uongozi maendeleo mMeatu yaongezeke

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *