JAJI WEREMA AFARIKI DUNIA WAKATI AKIPATIWA MATIBABU..

Aliyewahi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika Serikali ya Awamu ya 4, Mwaka 2009 hadi 2014, (AG), Jaji Fredrick Werema (69) amefariki Dunia wakati akipata matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) Dar es Salaam.


Kabla ya kifo chake, Werema aliwahi kuhudumu kama Wakili, Jaji katika Kitengo cha Biashara cha Mahakama Kuu na pia, aliwahi kufundisha kwenye Shule ya Sekondari ya Shaaban Robert Mwaka 1979 hadi 1980.

Mbali na taaluma ya sheria inayojulikana na wengi, Jaji Werema amewahi kuwa Mwalimu wa Shule ya Sekondari Shaaban Robert, jijini Dar es Salaam kati ya mwaka 1979 hadi 1980.

Sambamba na nafasi hiyo, pia amekuwa wakili tangu mwaka 1984 hadi 2006 na baadaye 2009 aliteuliwa kuwa AG, nafasi aliyohudumu hadi mwaka 2014 alipojiuzulu.

Pia, amewahi kuwa Jaji wa Mahakama Kuu katika Divisheni ya Biashara, Desemba 16, 2014, alijiuzulu nafasi yake akimweleza Rais Jakaya Kikwete kuwa anachukua uamuzi huo kwa kutoeleweka kwa Ushauri aliotoa juu ya sakata la ESCROW lililohusisha uchotwaji takriban Tsh. Bilioni 306 katika akaunti ya Tegeta Escrow.

sakata hilo lilisababisha Viongozi mbalimbali kupoteza nafasi zao wakiwemo Mawaziri Prof. Sospeter Muhongo na Prof. Anna Tibaijuka huku Andrew Chenge, William Ngeleja na Victor Mwambalaswa wakivuliwa nyadhifa za Uenyekiti wa Kamati za Bunge

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *