Israel yaapa kulipa Kisasi dhidi ya Iran

Mkuu wa majeshi ya Israel Herzi Halevi ameapa kuchukua hatua za kulipiza kisasi dhidi ya Iran baada ya shambulizi lake la mwishoni mwa wiki. Iran ilirusha zaidi ya makombora 300 na droni kuelekea Israel Jumapili usiku.

Awali Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu aliongoza kikao cha baraza la vita la serikali yake jana usiku ambacho kilidumu kwa saa tatu ILI kujadili hatua zinazoweza kuchukuliwa kujibu shambulizi hilo la Iran.

Kwa mujibu wa kituo cha utangazaji cha Channel 12 cha nchini Israel hatua zilizojadiliwa na baraza hilo la mawaziri la vita zilianzia kwa zile ndogo hadi zile kali zaidi. Kiliripoti kuwa Israel inalenga kuweka usawa kati ya kusababisha uharibifu nchini Iran lakini sio kuzusha vita vya kikanda, Mshirika mkuu wa Israel, Marekani,ilisema haifahamu Mipango yeyote

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *