Iran Yavuka Kiwango cha Uzalishaji Uranium Kinachoruhusiwa

Shirika la Umoja wa Mataifa la kufuatilia silaha za nyuklia limesema Iran imesindika idadi kubwa ya madini ya Uranium ambacho ni zaidi ya kilo 6,201.3 ikiwa ni ongezeko la kilo 675.8, nchi hiyo kwasasa imeongeza idadi ya shehena yake hadi kukaribia kiwango cha utengenezaji silaha, Jumatatu katika ripoti ya siri.

Ripoti hiyo imesema usambazaji wa madini ya Uranium ya Iran umefikia mara 30 zaidi ya kiwango kilichokubaliwa katika makubaliano ya mwaka 2015, kati ya Tehran na mataifa yenye nguvu duniani ili kupunguza program ya nyuklia ya Iran.

Mkurugenzi wa IAEA na mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kudhibiti silaha za nyuklia Rafael Grossi alionya mwezi uliopita kwamba Iran imekuwa na uranium iliyorutubishwa yenye kiwango cha kutosha kwa mabomu kadhaa ya nyuklia iwapo itaamua kutengeneza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *