Iran yaipiga kufuli Dola ya Marekani

Serikali ya Iraq imepiga marufuku matumizi ya dola ya Marekani kwa manunizi na matumizi rasmi kuanzia mwezi Januari, 2024. Hayo ni kwa mujibu wa Mazen Ahmed, mkurugenzi mkuu wa uwekezaji na uhamisho wa fedha katika Benki Kuu ya Iraq (CBI).


Hata hivyo, dola zozote, zitakazowekwa kuanzia 2024 zinaweza tu kutolewa kwa sarafu ya ndani Iran.
Taarifa ya Benki Kuu ilisema kuwa marufuku ya dola itatumika tu kwa akaunti zinazopokea uhamisho kutoka nje ya nchi.


Benki nyingi za ndani nchini Iraq tayari zimekuwa zikithibiti uondoaji wa dola katika kipindi cha miezi iliyopita, hali inayozidisha uhaba wa fedha hizo za kigeni.


Mnamo Julai, Hazina ya Marekani ilizipiga marufuku benki 18 za Iraq kwa madai ya kuwezesha miamala ya dola za Marekani hadi Iran, nchi ambayo imewekewa vikwazo vya kiuchumu na Marekani. Kutokana na hali hiyo, takriban theluthi moja ya benki za Iraq zimepigwa marufuku kuwezesha uhamisho wa dola.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *