Mlinzi wa kati wa Simba Sc, Henock Inonga ameruhisiwa kutoka hopsitali jana baada ya kupata matibabu kufuatia kuumizwa na winga wa Coastal Union, Haji Ugando katika mchezo wa wao Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Coastal uliopigwa jana Septemba 21, 2023.

Daktari wa timu, Edwin Kagabo amesema Inonga alichanika juu kidogo ya kifundo cha mguu na ameshonwa nyuzi 13 katika jeraha hilo na tayari ameruhisiwa kurudi nyumbani.
Wakati huo huo Kiungo Mshambuliaji wa Coastal Union Haji Ugando amemuomba radhi Beki wa Simba SC Henock Inonga Baka kwa kitendo kisicho cha kiungwana alichomfanyia wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa jana Alhamis (Septemba 21), Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.
Ugando alimchezea rafu Beki huyo kutoka DR Congo iliyosababisha kutolewa nje kwa kadi nyekundu, huku Inonga akikimbizwa Hospitali ya Rufaa ya Temeke.