Beki kipenzi cha mashabiki wa klabu ya Simba SC , Henock Inonga kupitia Mtandano wake wa kijamii wa Instagram amepost Emoji za machozi katika Insta Story zikiambatana na ujumbe wa neno Bye pamoja na saluti za kutosha chini yake akimalizia na Upinde wa mshale.

Hii inakoleza tetesi zinazosema kuwa huenda Mchezaji huyo hatakuwa tena sehemu ya kikosi cha wanamsimbazi kwa msimu ujao hivyo kwa post yake inaweza kuashiria ukweli wa tetesi hizo kuwa mchezaji huyo huenda akaondoka klabuni hapo mwishoni mwa msimu huu.
