Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

India yaipatia Tanzania gari 10

Serikali kupitia Wizara ya Afya ipo katika hatua za mwisho za kuanzisha mfumo wa Taifa wa uratibu na matumizi ya magari ya kubebea wagonjwa (Ambulance) ili kurahisisha upatikanaji wa huduma za dharura kwa haraka.

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu ameyasema hayo leo Octoba 4, 2023 wakati wa hafla ya kupokea magari 10 ya kubebea wagonjwa yenye thamani ya Shilingi Bil. 1.1 kutoka Serikali ya India.

Wakati akipokea magari hayo Waziri Ummy amesisitiza magari yote ya Serikali ya kubebea wagonjwa (Ambulance) lazima yawe yamekatiwa Bima ili kulinda magari hayo na yaendelee kufanya kazi.

Vilevile Waziri Ummy amewataka madereva wa magari yote ya kubebea wagonjwa kuzingatia sheria, taratibu na matumizi sahihi ya kuendesha magari hayo ikiwemo kupakia wagonjwa tu na sio vinginevyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *