Mkuu wa Shirika la Fedha Duniani IMF, Kristalina Georgieva ametahadharisha kuhusu ushuru mpya uliotangazwa na Rais wa Marekani, Donald Trump kwa bidhaa zinazoingia Marekani kuwa unaweza kusababisha hatari kubwa kwa uchumi wa dunia.
Georgieva amesema hayo imuda mfupi baada ya Trump kutangaza viwango vipya vya ushuru kwa bidhaa zinazoingizwa nchini humo, wa asilimia 34 kwa China na asilimia 20 kwa Umoja wa Ulaya, EU, ambapo kiwango cha chini cha ushuru wa forodha ni asilimia 10.

Amesema, ni muhimu kuepuka vitendo vinavyoweza kudhuru zaidi hali ya uchumi wa dunia, kwani hatua hiyo ya Marekani imezusha hofu na ukosoaji duniani kote huku nchi kadhaa zikisema zitalipiza kisasi.
Trump anasema ushuru huo kwa bidhaa zinazoingia Marekani ni wa kulipiza kile ambacho mataifa husika yamekuwa yakiifanyia Marekani kwa muda mrefu na kwamba unalenga kurejesha uzalishaji wa ndani na kulinda ajira za Wamarekani.
