Na Afarah Suleiman, Babati – Manyara.
Jumla ya watoto elfu 14 huzaliwa Tanzania na ugonjwa wa Selimundu, huku asilimia 7 wakipoteza maisha Kati yao kwa kuchelewa kutambuliwa kuwa wameathirika na ugonjwa huo.
Idadi hiyo imetajwa na wataalam wa afya katika mafunzo maalum ya kuwajengea uelewa Waandishi wa Habari Mkoani Manyara, kwa lengo la kufikisha elimu sahihi kwa jamii juu ya ugonjwa huo ambao ni wa kurithi na usiosababishwa na imani zozote za kishirikina.

Daktari Bingwa wa magonjwa ya Watoto Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Manyara, Joshua Gidion amesema hali ya ugonjwa huo umetajwa kugubikwa na imani za kishirikina na kupelekea jamii kuchelewesha waathirika kupatiwa matibabu kwa wakati.

kwa mujibu wataalamu wamesema Duniani kote watu laki 3 hadi laki 4 huzaliwa na ugonjwa huo ambapo nchini Tanzania watoto elfu 14 huzaliwa na ugonjwa huo kila mwaka na 7% hupoteza maisha ikiwa watoto 15-20% wanakadiriwa kuwa na vinasaba vya sikoseli au selimundu.



