ILANI YA CCM ITAKAYOZINDULIWA NI SHIRIKISHI – DKT. SAMIA

Raisi Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema Ilani ya CCM inayoenda kuzinduliwa kesho imeshirikisha Wananchi, Mashirika na Taasisi mbalimbali Nchini.

Akizungumza leo Kwenye Mkutano Mkuu wa Chama hicho ambacho kimekutanisha Wajumbe na Wadau mbalimbali wa Chama kilichofanyika katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma, ambapo amesema, yapo mashirika, makundi mbalimbali na vyuo vya ngazi ya juu wameshiriki katika kuchambua Ilani hiyo.

“Ilani tunayokwenda nayo imeandaliwa kwa weledi mkubwa na kwa kushirikisha Wananchi wenyewe, taasisi, Asasi za kiraia na makundi mengine mengi kutoka maeneo tofauti tofauti”, amesema

“Aidha Ilani yetu imeainisha vipaumbele vya chama ambapo muda utakapo wadia vitawekwa bayana hapa na kama ambavyo mnafahamu Ilani kuu ya chama hii tunayoimalizia iliakisi vipaumbele”. Amesema Dkt. Samia.

Dkt. Samia amesema kabla ya kuwasilishwa kwa Ilani hiyo chama kimeamua kufanya mapitio ya utekelezaji wa ilani iliyopita kwa miaka mitano.

“Tumeona kwanza kabla ya kuileta kwenu Ilani hii tumeona kwanza tufanye mapitio wote kwa pamoja leo hii na kesho tutaiwasilisha Ilani hii tunayo kwenda nayo, ila leo tujue inavitu gani ndani”, amesema.

“Matarajio yangu ni kuwa baada ya kupokea taarifa za Serikali za utekelezaji wa Ilani hii ya uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 pamoja na uzinduzi wa ilani hii mpya, Wajumbe wote wa Mkutano Mkuu kwa pamoja tutabeba jukumu la kufikisha na kutangaza Ilani kwa Wananchi wakati utakapofika”. Ameseka Dkt. Samia

Hata hivyo amesema jukumu hilo litakuwa sambamba na kutangaza mafanikio yaliyofikiwa na CCM katika ilani inayomalizika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *