IDADI YA WAJAWAZITO WALIOHUDHURIA KLINIKI YAFIKIA MILIONI 2.1

Na Gideon Gregory – Dodoma.

Imeelezwa kuwa katika kipindi cha Mwezi Julai 2024 hadi Machi 2025 idadi ya Wajawazito waliohudhuria Kliniki imeongezeka na kufikia Milioni 2.1 angalau mara moja kati ya wajawazito Milioni 2.07 waliotarajiwa.

Hayo yameelezwa leo Juni 2, 2025 Bungeni Jijini Dodoma na Waziri wa Afya, Jenista Mhagama wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2025/26.

“Ongezeko hilo la matumizi ya huduma za kliniki wakati wa ujauzito limetokana na utoaji wa elimu, uwepo wa vituo vya kutolea huduma za afya karibu na wananchi, pamoja na utekelezaji wa mwongozo wa huduma muhimu wakati wa ujauzito,”amesema.Aidha, ameongeza kuwa 

kwa kuzingatia vigezo vya Umoja wa Mataifa, Wizara hiyo imeendelea kuimarisha huduma wakati wa kujifungua na kuhamasisha wajawazito kujifungulia katika vituo vya kutolea huduma za afya.

“Katika kipindi cha Julai 2024 hadi Machi 2025, jumla ya wajawazito Milioni 1.9 walijifungua na kati yao, wajawazito Milioni 1.6 sawa na asilimia 87.4 walijifungulia kwenye vituo vya kutolea huduma,”ameongeza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *