Wizara ya Afya Nchini Uganda, imesema idadi ya watu walioambukizwa ugonjwa wa Ebola imepanda na kufikia tisa, ikiwa ni wiki kadhaa tangu ilipobaini kisa cha kwanza cha maradhi hayo hatari kwa Mwanadamu
Taarifa ya Wizara hiyo, imesema Wagonjwa saba kati ya tisa wanapatiwa matibabu kwenye Hospitali moja ya jijini Kampala na mgonjwa mwingine amelazwa katika Hospitali ya mji wa Mbale karibu na mpaka na Kenya.
“Mtu mmoja ndiye amekufa tangu janga hilo lilipozuka ila wagonjwa wote wanane wako kwenye hali nzuri, na watu 265 waliowahi kukutana na wagonjwa hao wamewekwa karantini,” ilieleza taarifa ya Wizara ya Afya.
Kwasasa Uganda inatoa chanjo ya majaribio dhidi ya kirusi hicho cha Ebola klichoanzia Sudan, ambayo iliidhinishwa kutumika kwa muda na Shirika la Afya Duniani WHO, Januari 2025.