IBRAHIM TRAORE: SOJA MTATA MWENYE UTATA

Kapteni Ibrahim Traore wa Burkina Faso, ndiye kiongozi mdogo zaidi wa eneo hilo na mwanajeshi mkakamavu ambaye amejizolea umaarufu kutokana na misimamo yake na aina ya uongozi wake akiutanguliwa mbele Uafrika.

Kapteni Traore alimpindua Luteni Kanali Paul-Henri Damiba Septemba 30, 20222 ikiwa ni mapinduzi ya pili ya kijeshi kwa mwaka huo ambayo yalitabiriwa kupunguza kasi ya mpito kuelekea utawala wa kiraia.

Traore, aliyezaliwa mwaka 1988, alianza kazi yake ya kijeshi mwaka wa 2009 na amehudumu katika vikosi mbalimbali mashariki na kaskazini mwa Burkina Faso.

Umahiri wake katika kuongoza na aina ya maamuzi anayoyachukua ili kulinda utamaduni wa mwafrika na kukuza uchumi wa Taifa lake, umewashangaza wengi.

Hivi karibuni Traoré alipiga marufuku mawigi yenye asili ya ukoloni wa Kiingereza na Kifaransa kwa majaji, akiitaja kama hatua muhimu ya kuondoa urithi wa wakoloni kwenye mfumo wa Mahakama nchini humo.

Alisema, haoni kama imeongeza nguvu kwenye mfumo wa Mahakama, bali inaendeleza utamaduni wa Waingereza na Wafaransa.

Ikumbukwe, katika baadhi ya  nchi nyingi za Afrika, majaji na mawakili bado wanavaa mawigi yenye asili ya ukoloni wa Uingereza ikiwemo Ghana, Kenya, Nigeria nk.

Traore anaendelexa maamuzi ya Nchi kama India na Pakistan, ambazo awali nazo zilikuwa koloni za Uingereza na sasa zimeachana na utamaduni wa mawigi katika mifumo yao ya sheria.

Hatua hii ya Burkina Faso, inasisitiza uamuzi wa kuimarisha utambulisho wa kitaifa na uhuru wa nchi ukiwa ni mfano wa wimbi jipya linaloendelea Afrika, ambapo baadhi ya nchi zinapitia upya urithi wa kikoloni na kuchagua mifumo inayolingana na mahitaji ya Wananchi wake.

Katika Miaka 2 ya Rais Ibrahim Traoré Madarakani, alikuza pato la Taifa la Burkina Faso kutoka takriban dola 18.8 bilioni hadi dila 22.1 bilioni. 

Amekataa pia mikopo kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na Benki ya Dunia, akisema, “Afrika haihitaji Benki ya Dunia, IMF, Ulaya, au Amerika.” 

Traore pia alipunguza mishahara ya mawaziri na wabunge kwa asilimia 30 na kuongeza mishahara ya watumishi wa umma kwa asilimia 50 na kulipa madeni ya ndani ya Burkina Faso. 

Alianzisha viwanda viwili vya kusindika nyanya, kikiwa ni cha kwanza kabisa nchini Burkina Faso na mwaka 2023, alizindua mgodi wa kisasa wa dhahabu, ili kuimarisha uwezo wa uchakataji wa ndani.

Alisimamisha utoaji wa dhahabu ya Burkina Faso ambayo haijasafishwa kwenda Ulaya na kujenga kiwanda cha pili cha kusindika pamba cha Burkina Faso kwani hapo awali, nchi ilikuwa na kiwanda kimoja pekee. 

Traore pia alifungua Kituo hiki cha Kitaifa cha Usaidizi cha kwanza kabisa cha Usindikaji wa Pamba wa Kisasa, akilenga kuwasaidia wakulima wa ndani wa pamba. 

Alitanguliza kilimo kwa kusambaza zaidi ya matrekta 400, tila 239, pampu 710 na pikipiki 714, ili kuongeza uzalishaji na kusaidia wadau wa vijijini. 

Kisha alihakikisha upatikanaji wa mbegu bora na pembejeo nyingine za kilimo unakuwepo, ili kuongeza pato la kilimo na hapo ndipo uzalishaji wa nyanya nchini Burkina Faso ukaongezeka kutoka tani 315,000 mwaka wa 2022 hadi tani 360,000 mwaka wa 2024. 

Uzalishaji wa mtama pia ulipanda kutoka tani 907,000 mwaka wa 2022 hadi tani milioni 1.1 mwaka wa 2024 na uzalishaji wa mpunga nao uliongezeka kutoka tani 280,000 mwaka 2022 hadi tani 326,000 mwaka 2024. 

Tukio jingine ni pale alipopiga marufuku operesheni za kijeshi za Wafaransa huko Burkina Faso na marufuku vyombo vya habari vya Ufaransa kuwafukuza Wanajeshi wa Urafansa waliopo nchini Burkina Faso. 

Serikali yake kwasasa inajenga barabara mpya, kupanua zilizopo, na kuboresha barabara za changarawe kuwa za lami, huku akijenga pia uwanja mpya wa ndege wa Ouagadougou-Donsin, unaotarajiwa kukamilika mwaka wa 2025.

Septemba 30 2022 aliwahi kunukuliwa akisema, “makubaliano yetu kwa pamoja yamesalitiwa na kiongozi wetu kwa jina luteni kanalii paul henri Damiba.

Kuzorota kwa hali ya usalama , hali iliotufanya kuchukua hatua, imetupiliwa mbali kutokana nah atua za kisiasa.’’Traore hakuishia hapo akaongeza kwamba, ‘’sikuamua kuchuku madaraka, nilichaguliwa wapo washirika wengine wanaowea kutuunga mkono iikiwemo Urusi. Wamarekani ni washirika wetu lakini pia tunaweza kushirikiana na Urusi.”

Kusuhu ghasia na mapinduzi Traore pia akabainisha kwamba ‘’Najua mimi nina umri mdogo sana zaidi ya wengi wenu hapa. Hatukutaka kilichotokea lakini hatukuwa na chaguo… kwa siku chache zilizopita , tumeusumbua usingizi wenu, tumesumbua usingizi wa wakaazi wa Ouaga kwa milio ya risasi. Hatukutaka hilo kiufanyika, lakini haya ndio Maisha.”

Ibrahim Traore, Kiongozi ambaye anapita katika reli za Thomas Sankara kwa kuwashangaza wengi jinsi anavyojongea kimantiki, akaingiza ingizo jipya kwa kupiga marufuku kifaransa kutumika kama lugha ya Taifa.

Ipo hivi: Serikali ya Burkina Faso ilipitisha mswada wa kurekebisha Katiba ili kuweka lugha za taifa kama lugha rasmi badala ya Kifaransa ambacho kimeshushwa kwenye daraja la lugha ya kazi nchini humo.

Kilichofuata ni Traore kutangaza kuondoa Kifaransa kama lugha rasmi ya nchi hiyo na kuwa lugha ya kufanyia kazi, hatua ambayo ilikuja kutokana na mzozo uliokuepo baina ya Taifa hilo na lile la Ufaransa.

Ripoti ya Baraza la Mawaziri ilibainisha kwamba muswada huo ulikuwa ni sehemu ya utekelezaji wa moja ya dhamira kuu za mpito ambayo inajumuisha kuanzisha mageuzi ya kisiasa, kiutawala na kitaasisi kwa nia ya kuimarisha utamaduni wa kidemokrasia na kuunganisha utawala wa sheria.

Ikumbukwe kwamba, tangu Kapteni Traoré aingie madarakani, Burkina Faso imejitenga na Ufaransa, ambaye mkoloni wa zamani na mshirika wa kihistoria wa Taifa hilo, huku ikiimarisha uhusiano wake na Urusi.

Burkina Faso ni nchi ya Afrika ya Magharibi isiyo na pwani kwenye bahari yoyote, ikipakana na nchi za Mali upande wa kaskazini, Nigeria upande wa mashariki, Benin, Togo, Ghana na Ivory Coast upande wa kusini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *