Kamanda wa Polisi Tanzania, IGP Camilius Wambura amewataka wanaoandaa maandamano Nchi nzima ili kuiangusha Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya awamu ya sita kabla ya mwaka 2025 wakome na wasitishe uchochezi huo na kusisitiza kuwa huo ni uhaini na hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
Amesema hayo leo Jijini Dar es salaam baada ya taarifa hizo zilizoanza kusambaa Jumatano 10 Agosti 2023 katika mitandao ya kijamii zinazohusisha kundi la Watu wanaoandaa maandamano ya kuiangusha Serikali.
“Huu ni Uhaini jambo la kwanza ni kuwahakikishia kwanza wakome kabisa na wasitishe matamshi yao ya kichochezi lakini jambo la pili niwape taarifa tu kwamba watachukuliwa hatua za kisheria kwa uchochezi wanaoufanya, Uhaini wanao-plan wote ni makosa ya jinai, niwaataarifu Jeshi letu la Polisi ni Jeshi imara sana wasitikise kiberiti ”