Mahakama kuu Kanda ya Dar es Salaam imepanga kutoa hukumu ya kesi ya kikatiba iliyofunguliwa na wabunge 19 wa viti maalum waliofukuzwa uanachama na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Ifikapo Disemba, 14 2023.
katika shauri hilo wabunge 19 wa viti maalum wakiongozwa na Halima Mdee wanapinga uamuzi wa baraza kuu la CHADEMA kutupilia mbali rufaa zao zilizopinga maamuzi ya kuondolewa uanachama kwa kile kiliichoitwa ‘usaliti’ kwa chama hicho kwa kuapishwa kutumikia nafasi ya ubunge wa viti maalum kupitia CHADEMA bila ridhaa halali ya chama.