Hukumu ya DP WORLD yaota mbawa

Mahakama kuu ya Tanzania Kanda ya Mbeya, imeahirisha kutoa hukumu ya kesi ya kikatiba ya kupinga mkataba wa Bandari baada ya Mwenyekiti wa jopo la majaji kupata dharura hivyo msajili wa Mahakama ameahirisha kesi hiyo hadi agosti 10, 2023.

Akitoa uamuzi huo Naibu msajili wa Mahakama kuu Tanzania Kanda ya Mbeya, Projestus Kahyoza, amesema hukumu hiyo ya kesi namba 5 ya mwaka 2023 itatolewa mnamo Agost 10.

Kesi hiyo ya kikatiba ya kupinga uwekezaji katika bandari ya Dar Es Salaam, ilifunguliwa katika Mahakama hiyo na wakili Emannuel Chengula, Alfonce Lusako,Raphael Ngonde na Frank Nyalusi kwa niaba ya wananchi, na kuwakilishwa na jopo la mawakili watatu wakiongozwa na Boniface Mwabukusi, huku upande wa serikali ukiwakilishwa na wakili msomi Mark Mukwambo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *